Lady Jaydee ‘Woman’ Album Comming Soon
Kupitia Instagram, Jide ameshare kile kinachoweza kuwa ndiyo cover rasmi
 la album hiyo. Muimbaji huyo mkongwe pia anatarajia kufanya concert 
kubwa kwaajili ya uzinduzi wa album hiyo.
“Natarajia kufanya concert kubwa kwaajili ya launch ya album ya Woman 
ambayo itakuwa ni mwishoni mwa mwezi March,” Jaydee alikiambia kipindi 
cha The Playlist cha Times FM.
“Na album yenyewe nategemea kuitoa mwezi ujao kwasababu siwezi tena 
kusubiri zaidi. Ilikuwa itoke mwaka jana mwishoni lakini kutokana na 
mipangilio kuwa haijakamilika, tukaisogeza mbele ili tufanye kitu kizuri
 zaidi kwa watu. Kwahiyo wajiandae kwa concert kubwa,” aliongeza.
Jide aliongeza kuwa kabla ya album haijatoka, ataachia nyimbo mbili alizowashirikisha wasanii kutoka nchi za Afrika.

No comments